ROBERTINHO AZISHTUKIA POWER DYNAMOS NA AL AHLY

KUELEKEA michezo yao miwili mikubwa ya kimataifa ule wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos na Robo Fainali ya African Football League ‘AFL’ dhidi ya Al Ahly kocha mkuu wa Simba Mbrazil, Roberto Olivieira ‘Robertinho’ ameshtukia jambo na anasuka bomu zito kwenye kambi yao.

Simba ambao wanaendelea na kambi ya maandalizi ya kabla ya msimu iliyopo Bunju, Dar wanatarajiwa kuvaana na Power Dynamos Septemba 15, mwaka huu kabla ya kuwaalika Al Ahly katika mchezo wa Robo Fainali ya AFL Oktoba 20, mwaka huu.ROBERTINHOKatika kuhakikisha kikosi chake kinakuwa tayari na ratiba ya michezo hiyo mikubwa, Robertinho ameomba michezo ya kirafiki kwa ajili ya kuongeza utimamu wa wachezaji wake kipindi hiki cha mapumziko kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa.

Katika mfululizo wa mechi hizo za kirafiki Simba jana Jumanne walipata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Cosmopolitan.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa na Moses Phiri dakika ya 14, Jean Baleke dakika ya 16, Willy Onana, Dakika ya 25, Aubin Kramo dakika ya 58 na Shabani Chilunda dakika ya 85.ROBERTINHORobertinho alisema: “Tuna michezo ya mashindano muhimu, nataka kuona kila mchezaji wangu anakuwa fiti kuelekea michezo hiyo. Nafurahia kuona maendeleo ya kikosi changu.

Acha ujumbe