Mechi za kuwania kufuzu Afcon mwakani zinaendelea leo hii ambapo timu ya Tanzania (Taifa Stars) itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Algeria ambayo yenyewe tayari imeshafuzu michuano hiyo.
Tanzania ipo nafasi ya pili kwenye kundi F akiw ana pointi 7, akifuatiwa na Uganda mwenye pointi 4, na wa mwisho akiwa ni Niger akiwa na pointi 2 pekee. Na Algeria akiwa na pointi 15.
Endapo Tanzania ikifuzu Afcon leo inakuwa ni mara ya tatu kufuzu ambapo mara ya kwanza kufuzu michuano hii ilikuwa 1980, 2019 lakini licha ya kufuzu imekuwa ni nadra kufanya vizuri kwenye michuano hiyo kutokana na ubora wa kikosi.
Kocha mkuu wa kikosi cha Stars Adel Amrouche amesema timu ipo vizuri na watahakikisha wanapata pointi ambazo zitawafanya wafuzu michuano hii leo majira ya saa 4:00 usiku.
Kutokana na wachezaji walioitwa na kocha huyo wadau mbalimbali wanaamini kuwa kitaleta ushindani hii leo kwani pointi 1 pekee inatosha kuwawazesha Stars kufuzu michuano hii.