Tanzania Yaipiga Mali Mpira wa wavu

Timu ya Taifa Mpira wa Wavu Tanzania (ALMASI KINGS) imeibuka na ushindi dhidi ya Timu ya Taifa ya Mali wa Set (3-1), Mashindano ya Afrika, mchezo uliomalizika muda mchache uliopita jijini Cairo nchini Misri.

Almasi Kings’ imekutana na upinzani mkali dhidi ya Mali ambapo mchezo ulikuwa wa vuta ni kuvute hasa Seti ya nne ambayo Tanzania imeibuka kwa ushidi wa point (24-26) na kuumaliza mchezo.tanzaniaTanzania iliuanza vyema mchezo huo kwa kushinda Set mbili za mwanzo ambazo vijana wa Almasi Kings walitawala na kushinda Set ya kwanza kwa point (18-25), Set ya pili point (22-25) kisha Mali wakajiuliza Set ya tatu na kuichukua kwa point (25-17).

Ushindi huo ni wa kwanza kwa ‘Almas Kings’ baada ya hapo jana kupoteza mchezo wao wa kwanza wa kundi B dhidi ya Chad kwa Set (3-0) Set ya kwanza (25-19),
Set ya pili (33-31) na
Set ya tatu (25-23). tanzaniaKatika huo mchezo Tanzania licha ya kupoteza walijikusanyia pointi 63 ambazo ziliiweka nafasi ya tatu kabla ya kucheza leo na Mali ambao jana walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Tunisia.

Tanzania (Almas Kings) kesho saa 14:00, watashuka Uwanjani kuwakabili Tunisia ambao nao wana kibarua leo dhidi ya Chad.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.