Robertinho Awaandaliwa Mipango Wazambia

KOCHA Mkuu wa Simba Mbrazili Roberto Oliviera ‘Robertinho‘ ameamua na sasa anataka kila faulo atakayoipata timu hiyo ndani ya 18 basi iwe bao.

Hiyo ni katika kuhakikisha timu yake inatumia vyema mipira ya kutenga watakayoipata nje ya 18 ya goli la wapinzani wake watakaokutana nao.

Kikosi cha Simba juzi kilirejea kambini kujiandaa na mchezo wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakaocheza dhidi ya Power Dynamos ya nchini Zambia.Robertinho

Robertinho alisema anataka kuona vijana wake wanazotumia vyema nafasi za mipira ya adhabu ya faulo wanazozipata nje ya 18 ya goli pinzani mara baada ya Ligi Kuu Bara kuanza wiki mbili zijazo.

Robertinho alisema kuwa timu yake imekuwa ikipata mipira mingi ya faulo, ambazo anaamini wangezitumia vyema, basi wangepata ushindi wa mabao katika michezo miwili ya ligi.

Aliongeza kuwa juzi jioni kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Bunju jijini Dar es Salaam aliwapa program hiyo ya kupiga faulo akiwatumia nyota wake Clatous Chama, Luis Miqquissone, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’, Hussein Mohammed ‘Tshabalala’ na wengine baadhi.

“Timu yangu bado naendelea kuiboresha lakini mara baada ya kurejea kambini jana (juzi) niliwapa program wachezaji wangu jinsi ya kupiga faulo.Robertinho“Hiyo ni baada ya kuona wachezaji wakishindwa kutumia nafasi nyingi za kupiga mipira hiyo ya kutenga nje ya 18. Kikubwa ninataka kila nafasi tutakayoipata ya faulo tunaitumia vyema katika kufunga mabao itakayopatikana ya faulo, wapo wachezaji ambao nimewaandaa kwa ajili ya kupiga mipira hiyo,” alisema Robertinho.

Acha ujumbe