AHMED ALLY AITAMBIA AL AHLY

KUELEKEA mchezo wa Robo Fainali ya mashindano ya African Football League dhidi ya mabingwa wa Afrika, Al Ahly, Meneja wa habari wa Simba, Ahmed Ally ametamba kuwa siku hiyo ndiyo watu watajua ubora wa kiungo wao mpya wa kimatafa wa DR Congo, Fabrice Ngoma kwani Al Ahly watakufa mapema sana.AHMED ALLYOktoba 20, mwaka huu Simba wanatarajiwa kuvaana na Al Ahly katika mchezo wa Robo Fainali ya mashindano hayo mapya ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika mwaka huu.

Ngoma amejiunga na Simba kutokea ndani ya kikosi cha Al Hilal ya Sudan ameanza vizuri msimu huu akiwa staa pekee mpya ambaye ameingia kikosi cha kwanza cha Robertinho na kutumika kwa dakika zote 180 za michezo ya Ligi Kuu Bara ambayo Simba wamecheza.

Ahmed Ally alisema: “Ngoma ni mchezaji wa daraja la juu sana, na amethibitisha hayo kwa kuangalia wasifu wa timu ambazo amewahi kupita, anawajua vizuri Al Ahly na Oktoba 20 ndiyo siku atathibitisha ubora wake.

Acha ujumbe