Ollie Watkins Amewaka

Mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa na timu ya taifa ya Uingereza Ollie Watkins ameendelea kuonesha makali yake ndani ya klabu hiyo na hiyo ni baada ya kufunga bao jana katika mchezo wa kombe la Uefa Conference League.

Mshambuliaji Ollie Watkins amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Aston Villa msimu huu, Huku ikiwa ni muendelezo ambao aliuanza msimu uliomalizika na msimu huu akionekana kuimarika zaidi.ollie watkinsRaia huyo wa kimataifa wa Uingereza alifanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza na hiyo ni kutokana na ubora ambao anakua anauonesha ndani ya kikosi cha Aston Villa chini ya kocha Unai Emery.

Mshambuliaji huyo kijana wa Uingereza mpaka sasa ana namba nzuri sana kwenye kikosi cha Aston Villa kwani amefanikiwa kufunga mabao 14 kwenye michezo 15 ambayo ameingia dimbani mpaka sasa.ollie watkinsKlabu ya Aston Villa ni moja ya vilabu vilivyofunga mabao mengi kwenye ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa wakifanikiwa kufunga mabao 23 mpaka sasa, Huku Ollie Watkins akiwa moja ya wachezaji waliofunga mabao mengi kwenye idadi hiyo.

 

Acha ujumbe