Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Gabriel Jesus na kiungo wa klabu hiyo Thomas Partey wamepata majeraha na watakosekana ndani ya klabu hiyo kwa wiki kadhaa.

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amethitibisha kua wachezaji wake wawili Gabriel Jesus na Thomas Partey wamepata majeraha ya misuli na watakosekana uwnajani kwa wiki kadhaa mbele.gabriel jesusKiungo Thomas Partey alipata majeraha mazoezini siku kadhaa nyuma jambo ambalo limemfanya kukosa mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Sevilla siku ya Jumanne usiku.

Mshambuliaji Gabriel Jesus yeye alionekana amepata majeraha madogo dhidi ya Sevilla katika ligi ya mabingwa barani ulaya, Lakini majeraha hayo yameonekana sio mepesi kwani yatamfanya mshambuliaji huyo kukaa nje ya uwanja kwa siku kadhaa.gabriel jesusKlabu ya Arsenal inatarajia kuwakosa wachezaji wake hao wawili ambao ni muhimu ndani ya kikosi chao, Wachezaji hao wamekua wakiandamwa na majeraha mara kwa mara jambo ambalo limefanya klabu ya Arsenal kufikiria kuingia sokoni kumsajili mshambuliaji mwezi Jnauari.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa