Osimhen Haondoki Napoli Januari

Mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen hataweza kutimka ndani ya klabu hiyo katika dirisha dogo la mwezi Jnauari kwa mujibu wa muendeshaji wa klabu hiyo bwana Meluso.

Muendeshaji wa klabu hiyo bwana Meluso ameeleza kua kwa umuhimu wa mchezaji kama Osimhen kuruhusiwa kuondoka kwenye dirisha dogo la mwezi Jnauari ni jambo ambalo haliwezekani na hakuna hiyo nafasi.osimhenMshambuliaji huyo amekua akihusishwa kuondoka ndani ya timu hiyo tangu katika dirisha kubwa la majira ya joto, Lakini hakufanikiwa kutimka na mpaka sasa amekua akihusishwa kuondoka haswa kutokana na taharuki iliyotokea klabuni hapo baina yake na timu hiyo.

Raia huyo wa kimataifa wa Nigeria inaelezwa yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na klabu ya Napoli ambapo mpaka sasa hawajafikia muafaka na ndio maana hakuna taarifa yeyote ya mshambuliaji huyo kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo.osimhenVictor Osimhen inaelezwa hana fuaraha ndani ya timu hiyo kwasasa a anataka kutimka ndani ya viunga vya Diego Armando Maradona, Lakini Napoli wao wanataka aongeze mkataba mpya jambo ambalo lina mvutano mpaka sasa.

Acha ujumbe