Winga wa klabu ya Wolverhampton na timu ya taifa ya Ureno Pedro Neto ameweka wazi kua bado yupo sana ndani ya klabu hiyo licha ya kuhusishwa kutimka klabuni hapo.

Pedro Neto akizungumza na wanahabari amesema anaipenda timu hiyo kwkaua klabu hiyo imemueka alipo kwasasa, Hii inaonesha kua mchezaji huyo hana mpango wa kutimka klabuni hapo hivi karibuni.pedro netoMchezaji huyo amekua akionesha kiwango kikubwa tangu ajiunge na timu hiyo, Lakini ndani ya msimu huu ubora wake umeongezeka na kufanya vilabu kadhaa kuwinda saini yake kuelekea dirisha dogo la mwezi Januari.

Kiungo huyo ameweka wazi kwasasa anafikiria kuipambania klabu hiyo kwakua yupo klabuni hapo, Lakini mambo ya mbeleni kwasasa hayapi nafasi kubwa hii kauli imezua maswali licha ya yeye kusema anaipenda klabu hiyo na yupo klabuni hapo.pedro netoKlabu ya Manchester United imehusishwa na Pedro Neto katika kipindi hichi ambacho winga wao Jadon Sancho anaweza kuachana na klabu hiyo, Huku mbadala sahihi ukionekana ni winga huyo wa kimataifa wa Ureno.

 JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa