KOCHA SINGIDA AUKUBALI MZIKI WA YANGA MAPEMA

KOCHA raia wa Brazil, anayeinoa Singida Big Stars Ricardo Ferreira amesema wazi kuwa mziki wa Yanga siyo mchezo, lakini wanakwenda kupambana kusaka alama tatu.

Ricardo alisema, Yanga ni timu ambayo imeonesha kuwa inaweza kupata ushindi kwenye muda wowote kutokana na aina ya wachezaji ambao wanao, lakini wamejipanga kutoa jasho na damu kusaka alama.

Kocha huyo aliongeza kwa kusema, kama walimpasua Namungo akiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, basi hata Yanga wanawezekana kwa sababu mpira ni ule ule tu.

“Yanga ni timu bora, ligi ya hapa Tanzania imekuwa sana na unaweza kuona namna ambavyo kuna ugumu wa kucheza na timu kama Yanga. Lakini tumejipanga kusaka alama.

“Wachezaji wao wote bora na wazuri sana, wanacheza kwa ubora na mbinu kubwa, lakini kwetu sisi kikubwa ni alama. Tuliwafungwa Namungo wakiwa kwao, basi hata Yanga wanaweza kufungwa wakiwa hapa,” alisema.

Kesho, Ijumaa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar, Yanga watakuwa wenyeji wa Singida Fountain Gate kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara.

Acha ujumbe