KOCHA wa Yanga raia wa Argentina Miguel Gamondi amesema kuwa, kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya Singida Fountain Gate FC ameandaa suprise kwa ajili yao.

Gamondi alisema amegundua kuwa kila mchezo ambao wanakwenda kucheza unakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wao wameshajua kuwa wao ni timu yenye ubora mkubwa.GamondiHivyo alichoamua kufanya kwa sasa ni kubadilika kwenye kila mechi ambayo atakuwa anacheza kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji lakini wakati huo wakiwa wamefanya kazi kubwa nyuma ya pazia.

“Tunajua kuwa tunakwenda kwenye mechi ngumu, ila tunakwenda kuwashangaza wapinzani wetu. Najua kuwa kila timu inafahamu sisi ni bora na inajipangaza zaidi kukutana na sisi.gamondi“Nafikiri kuna namna tumeshafanya kwenye uwanja wa mazoezi na kesho kila mmoja ataona, nina wachezaji bora na wazuri ambao nakuwa na uhuru wa kuchagua nani acheze wapi na kwa nini,” alisema Gamondi.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa