KOCHA wa Yanga, Miguel Gamondi ameeleza kuwa timu yake inapata ushindi mkubwa na kwenye mechi ngumu kwa sababu wachezaji na timu yake wanacheza kibingwa.

Gamondi alisema, anafurahishwa na namna ambavyo wachezaji na timu yake inavyocheza, hiyo inamfanya aone kabisa kuwa wanakwenda kutimiza malengo yao msimu huu.Gamondi“Timu inacheza kibingwa sana, kuna wakati unakuwa hauna wasiwasi kama kocha, kwenye mechi ngumu ugeuka na kuwa mechi rahisi. Hiyo kwetu inatia faraja kama benchi la ufundi.Gamondi“Unaweza ukaona mechi yetu na Azam FC, tulijua kuwa itakuwa ngumu sana kwa kuwa wapinzani wetu nao ni bora, lakini mwisho wa mchezo tunashinda na kuifanya mechi ionekane kama rahisi. Nawapongeza sana wachezaji wangu,” alisema Gamondi


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa