GAMONDI AANZA HESABU KALI ZA AZAM FC

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina amefichua kuwa akili yake kwa sasa ameielekeza katika mchezo wao ujao dhidi ya Azam baada kuvuna pointi tatu muhimu mbele ya Geita kwenye mchezo uliopigwa CCM Kirumba.

 

GAMONDI AANZA HESABU KALI ZA AZAM FC

Gamondi ametoa kauli hiyo kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo ambao umepigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Yanga inatarajia kucheza dhidi ya Azam FC Oktoba 25, mwaka huu kabla ya kugeukia michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo wamepangwa kundi D, zikiwemo na timu ya Al Ahly (Misri), Medeama (Ghana) na CR Belouizdad (Algeria).

Gamondi alisema kuwa baada ya kumalizana na Geita Gold, wanarejea katika mazoezi kuyafanyia kazi makosa yao kabla ya kuwavaa Azam katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara.

GAMONDI AANZA HESABU KALI ZA AZAM FC

Gamondi alisema kuwa kwa sasa mipango yake ipo kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa hivi karibuni waliteleza kwa kupoteza pointi tatu jijini Mbeya.

“Kwa sasa tunaangalia mechi iliyopo mbele yetu, tunafanya kazi mechi baada ya mechi, nimeona kundi letu katika Ligi ya Mabingwa Afrika lakini kabla ya kukutana na timu hizo tuna mchezo mgumu dhidi ya Azam ambao tunahitaji kuona tunapata matokeo.”

Kupoteza mechi moja haina maana tumepoteza malengo yetu, ligi ndiyo imeanza kuna mechi nyingi mbele yetu na lolote linawez kutokea, kwa sababu kufungwa na sare ni mambo ya kawaida katika mpira. Alisema kocha huyo na kuongea kuwa:

GAMONDI AANZA HESABU KALI ZA AZAM FC

Gamondi amesema kuwa hapendi kuahidi bali atafanya kazi kufikia malengo yao, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuendelea kusapoti timu yao kila inapokuwa na kufikia malengo.

Acha ujumbe