Imefichuka kuwa tayari viongozi wa klabu ya Al Ahly ya nchini Misri tayari wapo nchini kwa ajili ya kuandaa mazingira ya ushindi kuelekea mchezo wao wa ‘African Football League’ dhidi ya Simba.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Oktoba 20, katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya mashindano mapya ya African Football League.
Mchezo huo wa ufunguzi unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya kurudiana Cairo, Misri.
Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Tariq Hassani yupo nchini kwa ajili ya kutafuta moja ya Hotel ya nyota tano watakayofikia Al Ahly .
Katika taarifa hizo, kutoka Misri Mtendaji huyo ameongozana na msafara wa watu 20 watakaokuja kupiga Kambi Dar.
Taarifa hiyo ilisema kuwa pia viongozi hao wametua kwa ajili ya kuifuatilia katika mchezo wake wa Ligi Kuu Bara waliocheza jana dhidi ya Singida Big Stars uliopigwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa Liti Mkoani Singida.
“Tayari wapo viongozi wa Al Ahly wapo nchini kwa ajili ya kuandaa mazingira ya ushindi kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba. Msafara unaongozwa na Mtendaji wake Mkuu Tariq ambaye ameongozana na watu 20, waliofika kuandaa mazingira ya kufikia ikiwemo hotel na Uwanja watakaofanyia mazoezi.”
Pia viongozi hao baadhi huenda wakawepo katika mchezo wa ligi dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa leo (jana), Jumapili ili ni kuona mbinu za uchezaji watakazotumia, ilisema taarifa hiyo.
Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally alizungumzia hilo kwa alisema: “Kama uongozi nguvu zetu zimeelekeza katika mchezo wa ligi dhidi ya Singida Big Stars na baada ya hapo tutaelekeza nguvu kwenye mchezo dhidi ya wao Al Ahly.”