YANGA YAAPA KUTUSUA KIMATAIFA

Nyota wa Yanga, Maxi Nzengeli ametaja nguzo tano zinazowapa wachezaji nguvu ya kupata matokeo kwenye mechi za kitaifa na kimataifa wawapo uwanjani.

 

Maxi ameweka wazi kuwa jeuri kubwa waliyonayo msimu huu inaletwa na ubora wa vitu vitano vikubwa ambavyo ni, Mungu, benchi bora la ufundi, kujituma kwa wachezaji, kujitolea kwa viongozi na sapoti ya mashabiki wao.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Yanga imetinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwenye mechi nne ambazo ni dakika 450 Yanga ilishinda mechi zote nje ndani ambapo dhidi ya ASAS FC kwa jumla ya mabao 7-1 dhidi ya AL Merrikh kwa jumla ya mabao 3-0.

Maxi ambaye amejiunga na Yanga msimu huu mpaka sasa amefanikiwa kuifungia Yanga mabao matatu kwenye ligi na ametupia mabao mawili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya ASAS FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Nyota huyo amesema watazidi kupambana kwenye mechi za ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika kupata matokeo chanya na kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo.

“Kikubwa ni Mungu ambaye anatupa nguvu ya kufanya kazi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza pia mazoezi kwa ajili ya kila mechi ni muhimu, hivyo baada ya mchezo tunarejea kwenye uwanja wa mazoezi kuanza maandalizi mengine.”

Benchi la ufundi ambalo tupo nalo wao wanatupa mbinu ambazo zinatupa matokeo. Bila kusahau uongozi ikiwa ni Rais Injinia Hers Said na mashabiki hawa ni muhimu tunapenda kuona wanajitokeza kwenye kila mechi.

Kwenye ligi Yanga ina pointi 12 baada ya kucheza mechi 5. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika ipo kundi D ikiwa na Al Ahly, Madeama na CR Belouizdad.

Acha ujumbe