Manuel Neuer golikipa na nahodha wa klabu ya Fc Bayern ya nchini Ujerumani amesema wana bahati sana kutokufungwa na nyota wa zamani wa klabu hiyo Roberto Lewandowski aliehamia kwa miamba ya Hispania klabu ya Fc Barcelona katika mchezo uliopigwa jana usiku katika dimba la Allianz Arena nchini Ujerumani.

Nyota huyo wa zamani wa Bayern munich amekua na kiwango bora toka amejiunga na klabu ya Barcelona ikiwa tayari ameshaingia kambani mara tisa kwenye mechi sita za kimashindano alizoingia uwanjani kabla yab mechi dhidi ya Bayern ambayo alishindwa kufua dafu kitu ambacho golikipa mkongwe Neur anakiona kama bahati kutokana na kiwango bora alichokua nacho mshambuliaji huyo tangu kuanza kwa msimu huu.

manuel neurerKwenye mchezo huo ambao Barca walipoteza kwa goli mbili kwa bila waliweza kutengeneza nafasi za magoli lakini hawakuweza kufunga na miongoni mwa nafasi hizo ni za Roberto lewandowski aliepata nafasi mbili lakini Manuel Neuer kwenye kiwango bora kabisa akaokoa na kumnyima staa huyo magoli mawili.

Bayern munich baada ya kushinda mchezo huo wanaweka rekodi ya kutokupoteza michezo 30 katika hatua ya makundi na kuendeleza ubabe wake dhidi ya Barcelona.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa