Bayern Munich wanaendelea kuchehemea katika ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga baada ya kulazimishwa suluhu leo mapema wakiwa nyumbani dhidi ya klabu ya Stuttgart.

The bavarians wamepata wakati mgumu katika michezo yao mitatu ya mwisho katika ligi kuu ya ujerumani baada ya kuambulia alama tatu katika michezo hiyo yote.

bayern munichBayern walianza kuchechemea katika mchezo dhidi ya Borussia Monchengladbach baada ya kusuluhu goli moja kwa moja baada ya mchezo huo walipata suluhu ya goli moja kwa moja tena dhidi ya Union Berlin kabla ya kusuluhu leo goli mbili kwa mbili na Stuttgart ikiwa sio ishara nzuri kwa mabingwa hao watetezi wa ligi hiyo.

Mwalimu Julian Nagelsmann ana kazi ya kufanya kuhakikisha timu hiyo inarudi kwenye kiwango kizuri ambacho wanabavarians wanatamani kuona timu yao ikiwa nacho ili kuweza kutetea taji lao na kufanya vizuri kwenye michuano mingine.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa