Simba imefanikiwa kupata ushindi wa magoli mawili kwa bila katika mchezo wa awali waligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Nyassa Big Bullets ya nchini Malawi katika mchezo uliopigwa katika dimba linalofahamika kama Bingu National stadium nchini humo.

Vijana hao wa Juma Mgunda wanapata matokeo dhdi ya mabingwa hao kutoka nchini malawi mara baada ya kulazimishwa suluhu katika mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kulazimishwa sare ya goli mbili kwa mbili na klabu ya KMC jijini Dar-es-salaam.

simbaSimba ambao wamekua wazoefu katika michuano hii sasa walipata goli lao la uongozi kupitia kwa mshambulia wao raia wa Zambia Moses Phiri akiwa anafunga goli lake la nne katika michezo minne aliyocheza hadi sasa huku goli la pili likifungwa na nahodha wa timu hiyo mkongwe John Raphael Bocco.

Klabu hiyo inapata matokeo mazuri ikiwa ugenini kitu ambacho kinawweza kuwakikishia kusonga mbele kwenye hatua nyingine ya michuano kwani imekua nadra sana kwa klabu hiyo kupoteza mchezo wakiwa katika dimba lao la nyumbani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa