Klabu ya Simba SC imemaliza kufanya maandalizi yote kuelekea mchezo wao wa leo hatua ya kwanza, wakiwa ugenini kucheza na Nyasa Big Bullets huko Lilongwe Malawi.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Nassib Mkomwa (@nassibmkomwa_)

Kwa upande wa mazoezi timu ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Bingu ambao utatumika kwenye mchezo huo, na hivyo Kocha Mkuu wa muda wa klabu hiyo Juma Mgunda alisema kuwa wachezaji wamejipanga vizuri na mchezo.

Simba SC Wapo Tayari Kuwapa Furaha Mashabiki

 

“Sitaki kutoa sababu ukikubali kuvaa gwanda wewe ni mwanajeshi, baada ya kuzungumza na wachezaji wanaelewa mashabiki wanataka nini, wanaelewa watanzania wanahitaji nini kutoka kwao, kwahiyo niwaambie tu vijana wanaelewa hilo na naamini kesho watajitoa kwaajili ya Simba Sports Club”. Alisema Mgunda.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania)

Wekundu wa Msimbazi mpaka sasa ndiyo timu pekee Tanzania yenye Rekodi nzuri kwenye mashindano ya kimataifa, wakiwa na rekodi ya kufika hatua ya Robo Fainali mara tatu, ambapo mara mbili klabu Bingwa na Mara moja Kombe la Shirikisho kwenye misimu mitano iliyopita.

Simba SC Wapo Tayari Kuwapa Furaha Mashabiki
Mshambuliaji wa Simba SC, Pape Sakho akifunga goli kwa mtindo wa baiskeli “Bicycle Kick” Mechi kati ya Simba dhidi ya ASEC Mimosas.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa