Sterling Kutimka Chelsea

Taarifa kutoka ndani ya Chelsea zinaeleza kua winga wa klabu hiyo Raheem Sterling yuko mbioni kutimka ndani ya klabu hiyo baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili.

Winga Sterling alijiunga na klabu ya Chelsea msimu wa 2022/23 akitokea klabu ya Manchester City ambako alikaa kwa misimu takribani sita, Kwasasa mchezaji hiyo anaelezwa kuanza mazungumzo na vilabu vingine ili aweze kutimkia huko kwakua haweza kusalia ndani ya klabu hiyo.sterlingKocha wa klabu hiyo Enzo Maresca alipohojiwa kuhusiana na suala la winga huyo alifunguka kwa kusema “Nilizungumza na Raheem faragha siku moja kabla ya mechi na City. Sina kitu kipya cha kumwambia… kwani nilikuwa wazi kabisa.”

“Iwapo anataka kuzungumza tena, nitamwambia kile nilichomwambia tayari.”

Kutokana na maelezo ya kocha Enzo Maresca ni wazi winga huyo anaondoka kwenye timu hiyo kwakua sio chaguo la mwalimu ambaye ni mpya ndani ya timu ya taifa ya Italia, Mpaka sasa imebaki wiki moja dirisha la usajili kuweza kufikia tamati hivo Sterling ana nafasi ya kutafuta timu nyingine ya kutimkia.

Acha ujumbe