Aliyekua kiungo wa klabu ya Barcelona Ilkay Gundogan amerejea klabu ya Manchester City baada ya kukaa nje ya klabu hiyo kwa muda wa mwaka mmoja pekee.
Gundogan ambaye ameitumikia Manchester City kwa takribani misimu saba aliondoka ndani ya Manchester City punde tu baada ya kumalizika kwa msimu wa mwaka 2022/23 na kujiunga na miamba ya soka kutoka nchini Hispania klabu ya Fc Barcelona, Ambapo ameitumikia kwa wa mwaka mmoja na kuamua kurejea Man City.Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki inaelezwa ameondoka ndani ya klabu ya Barcelona kulingana na sera ya klabu hiyo kutoka Catalans kuhakikisha inawapunguza wachezaji ambao wanachukua mishahara mikubwa, Kwani ikumbukwe klabu ya Barcelona inapitia wakati mgumu kifedha miaka ya hivi karibuni.
Baada ya Barcelona kuhitaji kiungo huyo aondoke ndani ya klabu hiyo klabu ya Manchester City ilifanya mawasiliano na wawakilishi wa kiungo huyo kama kuna uwezekano wa kumrudisha ambapo kocha Guardiola ndio alipitisha kurejea kwa kiungo huyo, Mapema leo nahodha huyo wa zamani wa Man City amekubali kurejea ndani ya viunga vya Etihad rasmi.Vilabu kadhaa kutoka Uturuki na Saudia Arabia vilikua vinahitaji saini ya Gundogan lakini kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani inaelezwa ameamua kurejea klabu yake ya zamani ya Man City, Sehemu ambayo alipata mafanikio makubwa akishinda kila taji ambalo alilishindani ndani ya klabu hiyo.