Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester City Ilkay Gundogan ameweka wazi kua ndoto yake ilikua kucheza klabu ya Fc Barcelona ambayo anaitumikia kwasasa.

Kiungo Gundogan ameweka wazi walifanya mazungumzo marefu ya kina na klabu ya Manchester City, Lakini mwisho wa mazungumzo ulikua mzuri kwani alifanikiwa kuondoka klabuni hapo na kwenda kujiunga kwenye klabu ya ndoto zake.gundoganKiungo huyo raia wa kimataifa wa Ujerumani alikua moja ya wachezaji pendwa kwenye kikosi cha Manchester City chini ya kocha Pep Guardiola, Kwani usajili wa kwanza wa kocha Guardiola klabuni hapo ulikua wa Mjerumani huyo.

Kiungo huyo aliondoka klabuni hapo kama nahodha ambaye alikua na mchango mkubwa kwa klabu hiyo kutwa mataji matatu ndani ya msimu mmoja ambapo walivunja rekodi ya majirani zao klabu ya Manchester United.gundoganManchester City inaelezwa kua walihitaji kuendelea kupata huduma ya Gundogan lakini kiungo alikua na lengo moja tu nalo ni kutimiza ndoto yake ya muda mrefu akiwa kijana mdogo kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya Hispania klabu ya Barcelona.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa