Coutinho Atimkia Qatar

Kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool, Barcelona na Bayern Munich Philipe Coutinho ametimkia klabu ya Al Duhail ya nchini Qatar kwa mkopo wa msimu mzima kutokea Aston Villa.

Kiungo Coutinho atakipiga nchini Qatar katika klabu ya Al Duhail inayoshiriki ligi kuu nchini humo mpaka msimu huu utakapomalizika ambapo dili hilo lilikubalika na mchezaji kwa siku kumi nyuma.coutinhoKiungo huyu wa kimataifa wa Brazil alihitajika na klabu ya Besiktas ya Uturuki pia lakini alikataa ofa ya klabu hiyo na kuamua kujiunga na klabu hiyo kutoka nchini Qatar.

Licha ya mchezaji huyo kukubaliana na klabu ya Al Duhail siku kumi nyuma lakini klabu ya Aston Villa inaelezwa ndio imepambania kwa kiasi kikubwa dili hili kukamilika na kiungo huyo kutimkia Qatar.coutinhoKiungo Philipe Coutinho aterejea ndani ya klabu ya Aston Villa ambapo mkopo wake utakua unamalizika kwakua bado ana mkataba wa na klabu hiyo, Hivo kinachosubiriwa ni kama mchezaji huyo atacheza vizuri Qatar na kuishawishi Villa kumrejesha.

Acha ujumbe