Coutinho Akanusha Tetesi Zinazoenea Anataka Kuondoka Aston Villa

Kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool na Barcelona kwasasa akikipiga katika klabu ya Aston Villa Philippe Coutinho amekanusha tetesi za kua amepanga kuondoka katika klabu hiyo.

Kiungo huyo ambaye alijiunga na klabu hiyo mwezi Januari msimu uliomalizika akiungana na mchezaji mwezake wa Liverpool ambaye alikua kocha klabuni hapo Steven Gerrard kabla ya kutimuliwa, Baada ya Gerrard kutimuliwa ilisemekana mchezaji huyo alitaka kuondoka klabuni hapo.coutinhoKiungo Philippe Coutinho amefafanua kupitia ukurasa wake wa Instagram kua taarifa zinazoenezwa kua alitaka kuondoka kwenye klabu hiyo ni za uongo na watu wazipuuze, Kwani hajawahi kua na mzungumzo yoyote na klabu ya kuomba kuondoka klabuni hapo.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye alicheza soka lake kwa kiwango bora kabisa katika klabu ya Liverpool, Lakini tangu aondoke klabuni hapo kuelekea Barcelona hakuwahi kurudisha ubora wake aliokua nao ndani ya Liverpool.coutinhoTaarifa za ndani zinaeleza kua Coutinho aliingiwa na hofu baada ya kufukuzwa kwa aliekua kocha wa klabu hiyo Steven Gerrard, Hivo mchezaji akaona kama hataweza kupata nafasi ndani ya klabu hiyo lakini yeye mwenyewe amekanusha taarifa hizo na kusema hizo ni habari za uongo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.