Fiorentina Yamuacha Nico Gonzalez Huku Mazungumzo Na Juve Yakiendelea

Nico Gonzalez hatahusika katika mchezo wa leo dhidi ya Puskás Akadémia FC, huku Juventus wakiendelea kushinikiza kumsajili winga huyo wa Argentina kutoka Fiorentina.

Fiorentina Yamuacha Nico Gonzalez Huku Mazungumzo Na Juve Yakiendelea
Mkufunzi wa Fiorentina Raffaele Palladino hajamjumuisha Nico Gonzalez kwenye kikosi chake kwa ajili ya mechi ya mchujo ya leo ya Conference dhidi ya Puskás Akadémia FC.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Winga huyo wa Argentina tayari alikosa mchezo wa ufunguzi wa Serie A msimu huu dhidi ya Parma wiki iliyopita. Anajitahidi kuondoka Stadio Franchi na kujiunga na Juventus.

Fiorentina Yamuacha Nico Gonzalez Huku Mazungumzo Na Juve Yakiendelea

Kulingana na La Gazzetta dello Sport, mkurugenzi wa Juventus Cristiano Giuntoli alituma ofa iliyoboreshwa kwa Nico jana usiku, kutoka €30m hadi €32m, ikijumuisha nyongeza.

Kuna taarifa hata hivyo, zinadai kuwa Fiorentina inaendelea kudai €40m.  Nico mwenye miaka 26, alijiunga na Fiorentina kwa mkataba wa €26m kutoka Stuttgart mnamo 2021.

Ana mabao 38 na asisti 19 katika mechi 125 za Serie A akiwa na Tuscans kwenye Serie A. Mkataba wake Stadio Franchi unamalizika Juni 2028.

Fiorentina Yamuacha Nico Gonzalez Huku Mazungumzo Na Juve Yakiendelea

Juventus walimtangaza Pierre Kalulu kutoka Milan jana na pia wanashinikiza kumsajili Teun Koopmeiners kutoka Atalanta.

Acha ujumbe