Rais wa klabu ya Fc Barcelona Joan Laporta amesema kua hana wasiwasi na mustakbali wa kiungo wao raia wa kimataifa wa Uholanzi Frenkie De Jong kwakua hana mpango wa kutimka.
Laporta amesema katika kitu ambacho kiungo huyo anaweza kukifanya cha mwisho kabisa ni kufikiria kuondoka klabuni hapo, Ameyaongea hayo wakati anaongea na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea klabuni hapo.Rais amesisitiza kua kiungo ana furaha sana klabuni na kila siku amekua akimuambia anatamani kuendelea kuitumikia klabu ya Barcelona, Hii inamaanisha kua kiungo ameendelea kushikilia msimamo wake ambao amekua nao kwa takribani misimu miwili sasa.
Kiungo huyo amekua akihusishwa kuondoka klabuni hapo kwa msimu wa tatu sasa na klabu ambayo amekua akihusishwa nayo ni Manchester United ya Uingereza, Lakini msimamo wake umekua mmoja wakati wote kua anahitaji kuitumikia klabu ya Barcelona kwa muda mrefu zaidi.Kutokana na msimamo ambao amekua akiuonesha kiungo Frenkie De Jong ndio umeweza kumpa rais Laporta hali ya kujiamini na kutokua na wasiwasi na mustakbali wa kiungo ambaye anawindwa kwa karibu na mashetani wekundu.