Fofana Huyoo Milan

Kiungo Youssouf Fofana kiungo wa kimataifa wa Ufaransa amefanikiwa kujiunga na klabu ya Ac Milan ya nchini Italia akitokea klabu ya As Monaco ya nchini Ufaransa.

Kiungo alishakubali ofa ya kujiunga na klabu ya Ac Milan wiki kadhaa zilizopita na kilichokua kinachelewesha dili hilo kumalizika ni klabu ya Ac Milan kutoa kiwango cha pesa ambacho Monaco ilikua inakihitaji, Lakini hatimae leo klabu hiyo imefanikiwa kutoa kiwango cha Euro milioni 25 na kupata saini ya kiungo Fofana.fofanaKiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu ya Monaco anaenda kujiunga na Ac Milan kuongeza nguvu kwenye safu yao ya kiungo ya miamba hiyo ya soka nchini Italia, Kutokana na ubora wa kiungo huyo ni wazi Milan wameongeza mtu sahihi kwenye safu yao ya kiungo.

Vilabu kadaa vilikua vikifukuzia saini ya kiungo Fofana baada ya kuonekana Ac Milan wanachelewa kulipa ada ya uhamisho wa kiungo huyo, Moja ya vilabu hivo ni Manchester United ambao mpaka sasa wanatafuta kiungo sokoni lakini faida ya Ac Milan waliyoipata ni kiungo huyo kuonesha nia ya kujiunga na Rossoneri.

Acha ujumbe