Sandro Tonali Kurejea dimbani mwezi huu

Kiungo wa klabu ya Newcastle raia wa kimataifa wa Italia Sandro Tonali atarejea uwanjani mwezi huu tarehe 28 kutokana na taarifa ambayo klabu yake imeitoa.

Sandro Tonali alikua nje ya uwanja tangu mwanzoni mwa msimu uliomalizika baada ya kubainika kujihusisha na michezo ya kubashiri akiwa kwenye ligi kuu ya Italia alipokua anaitumikia klabu  ya Ac Milan, Hivo sasa ni rasmi mchezaji huyo atarejea kuitumikia tena klabu ya Newcastle.sandro tonaliMwanzoni mwa msimu uliomalizika ilibainika kiungo huyo wa kimataifa wa Italia alikua anajihusisha na michezo ya kubashiri alipokua kwenye ligi kuu ya Italia, Ambapo alikua anaibashiria iliyokua timu yake Ac Milan baada ya kubainika na kufungiwa kutojihusisha na mpira wa miguu hatimae atarejea uwanjani mwishoni mwa mwezi huu.

Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani msimu mzima Sandro Tonali atarejea uwanjani kuitumikia klabu yake ya Newcastle ambapo alikua ameanza vizuri ndani ya klabu hiyo, Mashabiki wa klabu ya Newcastle wanamsubiri kwa hamu mchezaji huyo arejee uwanjani kutokana na ubora aliouonesha mwanzoni ndani ya kikosi hicho.

Acha ujumbe