Mchezaji wa timu ya Monaco na timu ya Taifa ya Ufaransa Youssouf Fofana amesema kuwa, atafanya kila awezalo ili kupata nafasi katika kikosi cha Ufaransa cha kuanzia kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar.

Fofana alicheza mechi yake ya kwanza ya Ufaransa dhidi ya Austria mwezi Septemba, lakini kiwango chake cha kuvutia kwenye Ligue 1 akiwa na Monaco kilitosha kumpa nafasi katika kikosi cha wachezaji 26 cha Didier Deschamps.

Majeraha ya viungo wenzake Paul Pogba na N’Golo Kante yanamaanisha kuwa anaweza hata kuanza kwa mabingwa hao watetezi wa kombe hilo, pamoja na mchezaji mwenzake wa zamani Aurelien Tchouameni.fofanaMchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anasema atafanya kila awezalo ili kupata nafasi miongoni mwa wachezaji wenzake wa Ufaransa kwa mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Australia siku ya Jumanne.

Fofana alisema kuwa; “Kama mgeni kwenye, tunakuja kugundua shindano hili kubwa, uwe na umri wa miaka 23 au 30, Kombe la Dunia la kwanza daima ni muhimu. Kama mshindani, nitafanya kila kitu kupata nafasi yangu katika kikosi cha kwanza, kama 26 lakini kila wakati kwa heshima kwa wachezaji wenzangu.”

Kuchelewa kwa Fofana kwenye kikosi kunaweza kuzua maswali kama yuko kwenye kiwango kinachohitajika ili kucheza Kombe la Dunia kwa Ufaransa, lakini mchezaji huyo anahisi uchezaji wake unajieleza.fofanaFofana aliongeza kwa kusema kuwa uwanjani ndio huzungumza, kocha alimuita kwa kuona kiwango chake na baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Austria kila mtu atathibitisha pia. Hivyo hana tena wakati wa kujiambia kama an afuraha au fahari kwani shindano linaanza sasa.

 

Ufaransa ilipata nguvu siku ya Jumamosi Raphael Varane aliporejea mazoezini kabisa Jumamosi.
Baada ya mechi yao na Australia, vijana wa Deschamps watamenyana na Denmark na Tunisia katika Kundi D huku wakipania kuhifadhi taji lao la Kombe la Dunia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa