Kocha wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui, amejiuzulu wadhifa wake miezi michache kabla ya kuanza kwa FIFA World Cup, akimaliza wiki kadhaa za tetesi kuhusu mustakabali wake. Regragui, aliyewahi kuifikisha Morocco nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar, ameeleza kuwa amechukua uamuzi huo kutokana na uchovu baada ya kuhudumu kwa karibu miaka minne.

Ripoti zinaeleza kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 23, Mohamed Ouahbi, anatarajiwa kuchukua nafasi ya kuinoa timu hiyo kuelekea Kombe la Dunia. Ouahbi alipata mafanikio makubwa baada ya kuiongoza Morocco kushinda Kombe la Dunia la vijana chini ya miaka 20 mwaka jana nchini Chile.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Regragui mwenye umri wa miaka 50 alikabiliwa na ukosoaji kutoka kwa baadhi ya mashabiki licha ya rekodi nzuri ya ushindi. Tangu achukue mikoba ya kuinoa Morocco mwezi Septemba 2022, aliiongoza timu hiyo kushinda mechi 36 kati ya 49, sare nane na kupoteza mechi tano pekee. Katika kipindi hicho, Morocco iliweka historia kwa kuwa taifa la kwanza kutoka Afrika kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia na pia kuweka rekodi mpya ya dunia ya ushindi mfululizo kwa timu ya taifa, ikishinda michezo 19 mfululizo kati ya Juni 2024 hadi Desemba mwaka huo.

Taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa Regragui alitaka kujiuzulu mapema baada ya Morocco kupoteza fainali ya Africa Cup of Nations dhidi ya Senegal mwezi Januari katika mashindano waliyoyaandaa wenyewe, ambapo walikuwa na matumaini ya kumaliza ukame wa miaka 50 bila ubingwa wa Afrika. Morocco inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki baadaye mwezi huu kujiandaa na Kombe la Dunia, wakicheza dhidi ya Ecuador mjini Madrid Machi 27 na Paraguay mjini Lens, France Machi 31. Katika Kombe la Dunia, Morocco itakuwa Kundi C pamoja na Brazil, Scotland na Haiti.

Nahodha wa Morocco, Achraf Hakimi, alimshukuru Regragui kupitia mitandao ya kijamii akisema kazi yake imewahamasisha wachezaji na taifa zima la Morocco pamoja na mashabiki milioni kadhaa duniani.


