Kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick, amekataa kufunga mjadala kuhusu uwezekano wa mshambuliaji Marcus Rashford kurejea Old Trafford baada ya kumaliza kipindi chake cha mkopo akiwa Barcelona.
Rashford, ambaye hajacheza kwa United tangu Desemba 2024, alimaliza msimu uliopita kwa mkopo katika Aston Villa kabla ya kujiunga na Barcelona msimu huu. Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amekuwa na msimu mzuri akiwa na vinara hao wa La Liga, lakini bado haijawa wazi kama klabu hiyo ya Hispania itatumia kipengele cha pauni milioni 26.1 kumchukua moja kwa moja.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hali hiyo imeacha mustakabali wa Rashford kuwa wa mashaka kuelekea dirisha la majira ya joto, huku pia akitarajia kushiriki na timu ya taifa ya England katika michuano ya FIFA World Cup itakayofanyika Amerika Kaskazini. Rashford bado ana mkataba wa miaka miwili na United, ambao unaweza kuongezeka thamani kwa asilimia 25 iwapo timu hiyo itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akizungumzia uwezekano wa Rashford kurejea, Carrick alisema “Nadhani kuna maamuzi yatakayofanyika kwa wakati wake kuhusu mambo fulani, na Marcus yuko katika hali hiyo. Kwa sasa hakuna kilichoamuliwa, lakini lazima maamuzi yafanyike wakati fulani.”
Katika hatua nyingine, United iliyo nafasi ya tatu inaweza kusogea karibu zaidi na kufuzu Ligi ya Mabingwa iwapo itashinda dhidi ya Chelsea wanaoshika nafasi ya sita katika mchezo utakaochezwa Stamford Bridge. Kiungo Kobbie Mainoo anaweza kurejea baada ya kupona majeraha, huku akiwa mmoja wa wachezaji muhimu chini ya Carrick.
Carrick pia alisisitiza kuwa yuko tayari kufanya kazi na wachezaji wote waliopo na kuwasaidia kuimarika, akisema “Kwa mtazamo wangu, yeyote aliye hapa nataka kufanya naye kazi, kumsaidia kuboresha kiwango chake. Kwa sasa tuna kikosi hiki, na wapo pia wachezaji walioko kwa mkopo kitakachotokea baadaye kitaamuliwa baadaye.”

