Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer, ameweka wazi msimamo wake kuhusu tetesi za kuondoka klabuni hapo, akisisitiza kuwa hana mpango wowote wa kuhamia kwingine licha ya kuhusishwa na kurejea jijini Manchester.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga na Manchester United katika miezi ya hivi karibuni, huku ripoti zikidai kuwa anaikosa sana nyumbani kwake. Hata hivyo, Palmer ameonekana kupuuzia madai hayo na kusisitiza kuwa yuko imara Stamford Bridge.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya kusumbuliwa na majeraha msimu huu, Palmer ameweza kufunga mabao tisa na kutoa asisti moja katika michezo 21 ya Ligi Kuu England, akionyesha mchango wake muhimu ndani ya kikosi cha Chelsea.

Akizungumza katika mahojiano na Waandishi wa habari Palmer alisema “Watu wanaongea tu. Nikiyaona, ninacheka. Ni kweli Manchester ni nyumbani kwangu na familia yangu ipo huko, lakini siikosi sana.”
Aliendelea kueleza kuwa “Labda nitaikosa kama sitakwenda kwa muda mrefu, lakini ninaporudi nahisi hakuna kinachonivutia huko. Sina mpango wa kuondoka Chelsea, bado tuna mengi ya kupigania.”
Palmer pia aligusia mipango ya klabu hiyo, akisema “Tuna nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Leeds United, na tukimaliza katika nafasi za Ligi ya Mabingwa, itatusaidia kusajili wachezaji tunaowahitaji. Nimezungumza na Reece James, anaamini mradi wa klabu asingesaini mkataba mpya mrefu kama asingekuwa na uhakika na mwelekeo wa timu.”

