Nini Hatma ya Mbeya City Ligi Kuu?

Klabu ya Mbeya City inatarajiwa kushuka dimbani hii leo kwaajili ya mchezo wa play off ya pili dhidi ya Mashujaa ya Kigoma ambapo mchezo huo utapigwa Dimba la Sokoine.

 

Nini Hatma ya Mbeya City Ligi Kuu?

Mchezo wa kwanza, Mbeya City walishangazwa na timu hiyo ambayo ilikuwa ikishiriki Ligi daraja la kwanza baada ya kupoteza kwa mabao 3-1 na kufanya mlima kuwa mrefu kwa vijana hao wa Mubiru.

Baada ya kushindwa kubakia Ligi kuu, timu hiyo ilicheza play off ya kwanza dhidi ya KMC ikashindwa kupata nafasi ya kubaki na sasa leo ndiyo hatma yao ya kucheza ligi kuu au ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Je leo hii Mashujaa kutangazwa kucheza ligi kuu msimu huu au Mbeya City atamzuia licha ya kuwa nyuma kwa mabao mawili.

Nini Hatma ya Mbeya City Ligi Kuu?

Hapa mwenye faida ni Mashujaa ambaye tayari ana mtaji wa mabao matatu huku kama Wanakoma kumwanya wanataka kusalia Ligi kuu msimu ujao inabidi washinde mabao zaidi ya mawili.

Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 10:00 jioni na mpaka kufikia saa 12:00 mbivu na mbichi zitakuwa zimejulikana. Nani kupanda ligi kuu na nani kushuka.

 

 

 

Acha ujumbe