Wolves Washuka Rasmi Daraja Baada ya Matokeo ya West Ham

Klabu ya Wolve  imethibitishwa rasmi kushuka daraja kutoka Premier League baada ya matokeo ya sare ya bila kufungana kati ya West Ham United na Crystal Palace. Matokeo hayo yameiacha Wolves ikiwa na alama 17, ikiwa nyuma kwa pointi 16 kutoka eneo salama huku zikiwa zimesalia mechi tano pekee.

Wolves Washuka Rasmi Daraja Baada ya Matokeo ya West HamKutokana na hali hiyo, kikosi kinachonolewa na Rob Edwards hakiwezi tena kufikia idadi ya pointi zitakazokiwezesha kubaki ligi kuu, hivyo kitarejea kwenye EFL Championship baada ya kudumu kwa miaka nane katika ligi ya juu. Hii ni mara yao ya kwanza kushuka daraja tangu mwaka 2012.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Wolves waliwahi kuwa na mafanikio makubwa baada ya kupanda daraja mwaka 2018, wakimaliza nafasi ya saba msimu wao wa kwanza, na kurudia nafasi hiyo pamoja na kufika nusu fainali ya UEFA Europa League msimu wa 2019/20. Hata hivyo, kupoteza wachezaji muhimu kulichangia kushuka kwa kiwango chao na kujikuta wakipambana chini ya msimamo.

Wolves Washuka Rasmi Daraja Baada ya Matokeo ya West HamMsimu huu ulianza vibaya kwa Wolves baada ya kupoteza mechi tano za mwanzo, na hali ikaendelea kuwa mbaya zaidi waliposhindwa kushinda hata mchezo mmoja kati ya mechi zao 19 za kwanza za ligi. Ingawa kulikuwa na maboresho baada ya mabadiliko ya benchi la ufundi, timu hiyo haikuweza kuonyesha dalili za kurejea katika ushindani.

Wolves Washuka Rasmi Daraja Baada ya Matokeo ya West HamAkizungumza baada ya kuthibitishwa kushuka daraja, kocha Rob Edwards alisema, “Ni kipindi kigumu kwa klabu na mashabiki wetu, lakini tutapambana kuhakikisha tunarejea tena kwa nguvu.” Wakati huo huo, kocha wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi, alikiri presha inayoongezeka akisema, “Bado tuna nafasi ya kupambana, lakini tunahitaji matokeo haraka kabla ya kuchelewa.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.