Klabu ya Wolverhampton imemfukuza kocha wake mkuu Bruno Lage raia wa Ureno baada ya timu hiyo kua na mwanzo mbaya wa msimu chini kocha huyo.
Wolverhampton wamemtimua mwalimu huyo baada ya kua na matokeo mabaya ndani ya msimu huu baada ya kuambulia alama sita tu katika michezo nane timu hiyo iliyocheza ikiwa imefungwa michezo minne,kutoka sare michezo mitatu na kushinda mchezo mmoja jambo ambalo halijawafurahisha mabosi wa klabu hiyo na kuamua kumtimua mwalimu huyo.
Mwalimu huyo aliechukua nafasi ya mreno mwenzake Nuno Espirito Santo klabuni mwaka 2021 amecheza mechi 46 za ligi hiyo huku akishinda michezo 16, akisuluhu michezo 9 na kufungwa michezo 21 ikiwa sio wastani mzuri sana lakini hali imekua mbaya zaidi msimu huu baada ya kuambulia alama sita michezo 8.
Licha ya kuongeza nguvu kwenye dirisha hili kwa wachezaji kama Matheus Nunez na Goncalo Guedes haijawasidia timu hiyo kufanya vizuri huku kocha huyo wa zamani wa mabingwa wa Ureno klabu ya Benfica akishindwa kabisa kupata matokeo mazuri.
Wolverhampton wanatazamia kutafuta mwalimu mpya atakaeleta mabadiliko katika timu hiyo mapema iwezekanavyo baada ya kuuanza msimu vibaya sana.