Bao la Toney Laitoa Kobe, Al Ahli Yatinga Fainali ya AFC Champions League

Klabu ya Al Ahli imefanikiwa kutinga fainali ya AFC Champions League Elite baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vissel Kobe katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jijini Jeddah.

Bao la Toney Laitoa Kobe, Al Ahli Yatinga Fainali ya AFC Champions LeagueMabingwa watetezi walijikuta nyuma mapema baada ya Yoshinori Muto kuifungia Vissel Kobe bao la kuongoza dakika ya 31, kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Katsuya Nagato na kupanguliwa vizuri na Yuya Osako kabla ya kumkuta Muto aliyefunga kwa urahisi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Al Ahli walirejea kwa nguvu kipindi cha pili, ambapo Galeno alisawazisha dakika ya 62 kwa shuti kali lililomshinda kipa Daiya Maekawa. Shinikizo lao liliendelea kuongezeka, huku wakikaribia kufunga mara kadhaa kupitia Ivan Toney na Franck Kessié.

Bao la Toney Laitoa Kobe, Al Ahli Yatinga Fainali ya AFC Champions LeagueDakika ya 70, Toney alihakikisha ushindi kwa kufunga bao la pili baada ya kutumia vyema krosi ya Galeno, akipenya katikati ya mabeki wa Kobe na kuipeleka timu yake mbele kwa ustadi mkubwa.

Bao la Toney Laitoa Kobe, Al Ahli Yatinga Fainali ya AFC Champions LeagueAkizungumza baada ya mchezo, kocha wa Al Ahli Matthias Jaissle alisema, “Tunajivunia kufika fainali tena mfululizo. Hili ni jambo maalum na heshima kubwa kwetu. Mechi ilikuwa ngumu na maamuzi madogo ndiyo yaliyoamua matokeo.”

Bao la Toney Laitoa Kobe, Al Ahli Yatinga Fainali ya AFC Champions LeagueKwa ushindi huo, Al Ahli sasa wanasubiri mshindi kati ya Shabab Al Ahli na Machida Zelvia ili kukamilisha fainali, huku wakilenga kuwa timu ya kwanza tangu Al Ittihad mwaka 2005 kutwaa taji hilo mara mbili mfululizo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.