Klabu ya Lazio imefanikiwa kutinga fainali ya Coppa Italia baada ya ushindi wa mikwaju ya penalti dhidi ya Atalanta katika mchezo mkali uliopigwa ugenini.
Ushindi huo pia unaweka historia kwa Lazio kwa kupata ushindi wao wa kwanza ugenini dhidi ya Atalanta kwenye mashindano hayo, na sasa watakutana na Inter Milan kwenye fainali.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa tangu mwanzo, huku Atalanta wakionekana kuanza vizuri licha ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha katika michezo yao ya hivi karibuni. Nafasi za wazi zilikuwa chache, ambapo Nicola Zalewski alikaribia kufunga lakini shuti lake lilipanguliwa, wakati Lazio walishindwa kuonesha makali makubwa kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili, Atalanta walifikiri wamepata bao kupitia Éderson lakini VAR ilikataa bao hilo kutokana na madhambi katika mchakato wa shambulizi. Baadaye, Lazio walipata bao muhimu kupitia Alessio Romagnoli aliyefunga kwa shuti kali baada ya kona ya Mattia Zaccagni, lakini Atalanta walijibu haraka kupitia Mario Pašalić kusawazisha.
Dakika za nyongeza zilikuwa na mvutano mkubwa huku bao la Giacomo Raspadori likikataliwa kwa kuotea, na kulazimisha mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti. Kipa wa Lazio, Edoardo Motta, aliibuka shujaa kwa kuokoa penalti nne mfululizo na kuwanyima Gianluca Scamacca na wenzake nafasi ya ushindi.
Kocha wa Lazio, Maurizio Sarri, alisifu kiwango cha wachezaji wake akisema “Tulionyesha uthabiti mkubwa na nidhamu ya hali ya juu. Ushindi huu ni matokeo ya juhudi za pamoja na imani tuliyonayo kama timu.” Kwa ushindi huo, Lazio sasa wanajiandaa kuivaa Inter Milan katika fainali itakayopigwa Mei 13, wakilenga kutwaa taji lao la nane la Coppa Italia, ikiwa ni mara ya kwanza tangu waliposhinda msimu wa 2018/19.

