TAARIFA ukufikie kuwa huenda mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Agosti 13 kati ya Simba na Yanga itakayopigwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar ikaamulia na Video Asistant Referee (video assistant referee) kwa mujibu wa Rais wa TFF Wallace Karia.

Var

Rais Karia alisema kuwa kwa sasa wapo kwenye mpango wa kujaribu na kutathimini gharama za kuendesha VAR na kama mambo yatakwenda vizuri  huenda ikatumika kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Akizungumzia ishu hiyo Karia alisema, kwa wele ambao walifuatiliwa Ligi Kuu ya Vijana wa U20 iliyomalizika wikiendi iliyopita kwenye uwanja wa Azam Complex watu walishuhudia kwa mara ya kwanza majaribio ya VAR kwenye mechi za nusu fainali na kwa bahati nzuri matokeo yamekuwa mazuri.

https://fb.watch/elhpbZ-aTe/ 

“Kama ambavyo Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alivyosema kuwa kuna mpango wa bajeti unafanywa kwa ajili ya VAR hapa nchini na kwenye ligi yetu. Sisi tumeona bora tuanze kufanya majaribio mapema kwenye ligi hizi za vijana.

VAR

“Matokeo yake yamekuwa mazuri kwenye mechi za ligi ya U20 ambayo kuna maamuzi yaliamuliwa kwa video assistant referee toka kwenye hatua ya nusu fainali. Tafsiri yake mambo yanakwenda vizuri na rasmi sasa mashindano haya ya vijana itakuwa inatumika kila msimu.

“Lakini pia tutaendelea kuangalia gharama na kufanya majaribio kwenye mechi zingine zinazofuata kama mambo yatakuwa mazuri basi watu wategemee kuona VAR ikitumika kwa msimu ujao kama ambavyo watu walikuwa wanapiga kelele,” alisema Karia.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa