Kampuni ya michezo ya kieletroniki EA Sports imeweka wazi cover itakayotumika kwenye ‘FIFA 23 Ultimate Edition’ na mchezaji nyota wa klabu ya PSG Kylian Mbappe na mwanadada nyota wa klabu ya Chelsea Kuoneka cover hiyo.

Kylian Mbappe hii ni mara yake ya tatu mfululizo kuweza kuonekana kwenye cover ya mbele ya FIFA, huku mwanadada Sam Kerr ikiwa mara yake ya kwanza, huku Nyota hao wawili wakiwa wamekaa juu ya jiwe nyuma kukiwa na dhahabu.

Kylian Mbappe

Kwenye utambulisho huo, EA Sports walitangaza kwamba uzinduzi wa FIFA 23 utafanyika July 20. Hli ndio litakuwa andiko la mwisho kupangwa kutoka kwa mwaka huu, lakini sio mchezo wa mwisho wa mpira wa miguu kwenye FIFA 23 the series ambazo zinatambulika kama EA Sports FC, kama inavyotambulika na wapenzi wengi wa mchezo huo.

Tarehe 20 July kupitia channel yao ya YouTube wamepanga kufanya uzinduzi wa FIFA 23 kuanzia saa 12 p.m. Na kuonesha  vipengere muhimi na baadhi ya taarifa kuhusu jinsi ya kulicheza na Teknolojia mpya ya muonekano.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa