Klabu ya Arsenal iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajiri wa Oleksandr Zinchenko baada ya kufikiana makubaliano na mchezaji huyo mwenye miaka 25 kwa mkataba wa miaka 4.

Arsenal wameandaa kiasi kinachokadiriwa kufikia £30million, pia watapaswa kulipa nyongeza ya £2million, ikiwa watafanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza .

Arsenal, Arsenal Kumvuta Zinchenko Kutoka Man City, Meridianbet

Kwa sasa Arsenal wamefanikiwa kukubaliana na mchezaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Ukraine, ila bado klabu yake ya Manchester City haijatoa majibu yoyote kwenye dau ambalo klabu hiyo ya London wamepelaka.

Ikiwa mambo yatakwenda sawa, Zinchenko atapswa kuondoka kambini kwenye michezo ya Pre-season na kurudi jijini London kwa ajiri kufanyiwa vipimo vya afya.

Usajiri wa Zinchenko ukikamilika, basi utakuwa usajiri wa tano kwenye kikosi chaArteta kwenye dirisha hili la kiangaz, kwani mpaka sasa wameshafanikiwa kuwasijiri Marquinhos, Matt Turner, Fabio Vieira na Gabriel Jesus.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa