Borussia Dortmund imeweka wazi kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo Sebastien Haller amegundulika kuwa na saratani ya tezi dume.

Haller Akutwa na Saratani ya Tezi Dume

Haller, 28, alijiunga na BVB mwezi Julai akitokea Ajax baada ya kufurahia msimu mzuri wa 2021-22, haswa katika Ligi ya Mabingwa ambapo alifunga mabao 11 katika mechi nane.

Lakini fowadi huyo aliugua wakati wa mazoezi ya pre-season katika klabu yake mpya, na uchunguzi wa kimatibabu uliofuata ulithibitisha ugonjwa huo.

“Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Sebastien Haller alilazimika kuondoka kwenye kambi ya mazoezi ya BVB huko Bad Ragaz, Uswizi, mapema kutokana na ugonjwa na tayari amesafiri kurejea Dortmund,” klabu hiyo ilieleza kwenye tovuti yake rasmi.

“Familia nzima ya BVB inamtakia kupona haraka tutafanya kila kitu katika uwezo wetu kuhakikisha anapata matibabu kikamilifu,” aliongeza kiongozi wa michezo wa Dortmund Sebastian Kehl.


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa