Klabu ya Tottenham Hotspurs imefanikiwa kuinasa saini ya Djed Spence kutoka katika klabu ya Middlesbrough kwa dau linaripotiwa kuwa ni pauni milioni 20.

Beki huyo wa alicheza michezo 42 ya Championship msimu uliyopita akiwa na Nottingham Forest kwa mkopo akiwa nguzo muhimu kwa klabu hiyo kupanda daraja la Ligi Kuu.

Spence anakuwa mchezaji wa 6 kusajiliwa na Spurs msimu huu baada ya Ivan Perisic, Fraser Forster, Yves Bissouma, Richarlison na Clement Lenglet aliyesajiliwa kwa mkopo

Baada ya kukamilika kwa usajili huo mchezaji huyo mzaliwa wa London na mhitimu wa akademi ya Fulham alisema: “Kucheza katika Premier League tena kwa klabu ya Tottenham ni ndoto kuwa kweli.”

“Kila mtoto kutoka kwenye akademi za hapa anatamani kucheza katika Ligi Kuu, ni klabu kubwa nitacheza katika Ligi ya Mabingwa vilevile kuna wachezaji wakubwa hapa nitacheza nao.”

Ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu ya Tottenham uliandika: “Karibu Spence,”


CHEZA KASINO MTANDAONI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa