UONGOZI wa timu ya Geita Gold FC unatarajia kuweka kambi nchini Burundi kwenye mji wa Bujumbura kwa ajili ya kujiandaa na mashindano yote yanayowakabili kwa msimu unaotarajia kuanza August.

Ofisa habari wa klabu ya Geita Gold, Hemed Kivuyo amesema kuwa kikosi cha timu hiyo kipo kwenye maandalizi ya safari ya kwenda nchini Burundi kuweka kambi. Pia alikazia swala la klabu hiyo kuendelea kufanya usajiri wa wachezaji wa kigeni ili kuimarisha kikosi cha timu hiyo.

Geita Gold FC
Geita Gold FC

“Timu itaweka kambi kwenye mji wa Bujumbura nchini Burundi mwanzoni mwa wiki ijayo, na itakaa huko kwa takribani wiki mbili, pia usajili unaendelea na kutakuwa na wachezaji kadhaa wapya wa kigeni .

“Sera ya Geita ni kuwapa kipaumbele wazawa, lakini kutokana na ugumu wa mashindano na idadi yake tumeona tuongeze nguvu zaidi kwa kuwaongeza wachezaji wa kigeni.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa