Arsenal Bado Wanaamini Taji la Ligi Kuu – Mikel Arteta

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema kikosi chake bado kina imani kubwa ya kutwaa ubingwa wa Premier League licha ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo muhimu wa mbio za ubingwa uliochezwa Jumapili.

Arsenal Bado Wanaamini Taji la Ligi Kuu – Mikel ArtetaLicha ya kipigo hicho, Arsenal bado wanaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi tatu juu ya Manchester City, ingawa wapinzani wao wana mchezo mmoja mkononi pamoja na kuwa katika kiwango kizuri kwa sasa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Matokeo hayo pia yanaongeza presha kwa Arsenal ambao wamepoteza michezo minne mfululizo katika mashindano ya ndani, hali iliyowafanya kushindwa kutwaa Kombe la Ligi na FA Cup, hivyo kuendeleza ukame wa mataji kwa miaka sita.

Arsenal Bado Wanaamini Taji la Ligi Kuu – Mikel ArtetaHistoria inaonekana kujirudia kwa timu hiyo ya London Kaskazini, kwani pia waliwahi kupoteza ubingwa mbele ya Manchester City katika misimu ya 2022/23 na 2023/24 licha ya kuwa na nafasi nzuri awali.

Hata hivyo, Arteta anaamini kikosi chake bado kina uwezo mkubwa, akisisitiza kuwa kiwango walichoonyesha katika mchezo huo kinaashiria matumaini makubwa kwa mechi zilizobaki.

Arsenal Bado Wanaamini Taji la Ligi Kuu – Mikel ArtetaAkizungumza baada ya mchezo, Arteta alisema “Ninaamini leo, niliamini Jumatano, na niliamini hata wiki iliyopita kwa sababu ninawaona wachezaji wangu kila siku na najua kiwango tulicho nacho. Kama walihitaji kuamini zaidi, basi sasa wanaamini zaidi.”

Aliongeza “Hii sasa ni ligi mpya. Tunaongoza kwa pointi tatu, wao wana mchezo mkononi. Kila kitu bado kiko wazi na tunajua tunakitaka kiasi gani, hatutasimama.”

Arsenal Bado Wanaamini Taji la Ligi Kuu – Mikel ArtetaArsenal wana ratiba inayonekana kuwa nafuu zaidi ukilinganisha na Manchester City katika michezo iliyosalia, lakini wanakabiliwa na changamoto ya ziada ya kushiriki pia Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu hiyo itakutana na Atletico Madrid katika hatua ya nusu fainali, wakilenga kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia yao. Licha ya ratiba ngumu, Arteta alisisitiza kuwa hakuna haja ya kuwahamasisha zaidi wachezaji wake kuelekea mwisho wa msimu. “Kama nitahitaji kuwahamasisha wachezaji ili washinde ligi wakiwa na mechi tano mkononi na nafasi ipo mikononi mwao, basi hiyo si sawa. Haijawahi kuwa hivyo, hata katika nyakati ngumu. Tutaendelea kupambana,” alisema Arteta.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.