Pep Guardiola Asema Ushindi Dhidi ya Arsenal Umeleta “Matumaini” kwa Manchester City

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Premier League uliochezwa Jumapili umeipa timu yake “matumaini” mapya katika mbio za ubingwa.

Pep Guardiola Asema Ushindi Dhidi ya Arsenal Umeleta “Matumaini” kwa Manchester CityGuardiola alionekana kuwa na shauku kubwa pembeni mwa uwanja katika mechi hiyo, lakini baada ya filimbi ya mwisho alipunguza umuhimu wa ushindi huo kwa neno moja tu  matumaini. Ushindi huo uliopatikana kwa bao la kipindi cha pili la Erling Haaland umepunguza pengo la pointi hadi tatu, huku City ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo, Guardiola alisema: “Kufurahia si neno sahihi. Ni sawa tu. Matumaini mechi hii imetupa matumaini. Hayo tu.” Aliongeza  “Niliwaambia wachezaji baada ya mchezo wafurahie ushindi, lakini wasipoteze umakini. Tupo karibu, lakini ukweli ni nani anaongoza ligi? Sio sisi. Hata kwa tofauti ya mabao, wao ni bora. Lakini bado tuna matumaini ya kuendelea kupigania ubingwa.”

Pep Guardiola Asema Ushindi Dhidi ya Arsenal Umeleta “Matumaini” kwa Manchester CityGuardiola pia alisifu ubora wa Arsenal, akisema: “Watu wanasema hawana mwendelezo, lakini ukiwaona wanavyocheza, wanavyopambana kwenye mipira ya juu, mipira ya pili na mipira iliyokufa, ni timu ya ajabu sana. Huwezi kuongoza ligi msimu mzima bila kuwa na ubora huo.”

Kocha huyo aliuita mchezo huo kuwa mfano bora wa soka duniani, akisema: “Huu ni mchezo bora wa kuitangaza ligi ya England duniani.”Katika mchezo huo, Erling Haaland alirejea kufunga bao la ligi kwa mara ya kwanza baada ya miezi miwili, akipambana vikali na mabeki wa Arsenal William Saliba na Gabriel Magalhães.

Pep Guardiola Asema Ushindi Dhidi ya Arsenal Umeleta “Matumaini” kwa Manchester CityGuardiola alitania kuhusu pambano hilo akisema: “Usingependa kuwa Haaland ukipambana na Saliba na Gabriel. Kwa kweli, ningependa kusoma kitabu tu.”

Kwa upande wake, Haaland alisema: “Hii ni kawaida, kuna mapambano mengi. Wengine wataamua kama nilishinda au la, lakini nilifunga bao, hivyo nilishinda wakati huo. Lilikuwa bao la muhimu na tukashinda.”

Guardiola pia aligusia uchovu wa mshambuliaji huyo kutokana na ratiba ngumu, akisema “Mchezaji mkubwa kama yeye kucheza kila baada ya siku tatu kwa miezi kadhaa si jambo rahisi kwa mwili.”

Pep Guardiola Asema Ushindi Dhidi ya Arsenal Umeleta “Matumaini” kwa Manchester CityMwisho, Guardiola alimpongeza nahodha Bernardo Silva ambaye anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka tisa. “Nikisema mengi siku moja nitalia. Ninasema tu asante kutoka moyoni. Ni mchezaji wa kipekee sana, hadhi ya ‘legend’ inamfaa kabisa,” alisema.

Manchester City wana nafasi ya kusawazisha pointi na Arsenal na hata kupanda kileleni iwapo watashinda dhidi ya Burnley Jumatano ijayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.