Kocha wa Everton FC, David Moyes, amemtetea kocha wa Arsenal FC, Mikel Arteta, kufuatia ukosoaji unaoendelea kuhusu mtindo wa uchezaji wa timu hiyo, hususan matumizi ya mipira ya adhabu (set-pieces) kama mbinu muhimu ya kufunga mabao.
Arsenal ambao wanaongoza msimamo wa Premier League wamekuwa wakikosolewa katika wiki za hivi karibuni kwa kutegemea zaidi mipira ya kona na mipira iliyokufa kama njia ya kupata mabao, jambo lililozua mjadala kuhusu mabadiliko ya mbinu katika soka la kisasa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, Moyes amepinga ukosoaji huo akisema hakuna tatizo kwa timu kutumia nguvu za mwili pamoja na mipira ya adhabu kama sehemu ya mkakati wa ushindi. Alisisitiza kuwa ni jambo la kawaida katika mchezo wa soka na halipaswi kuonekana kama dosari.
Aidha, Moyes alimpongeza Arteta ambaye aliwahi kuwa mchezaji chini yake Everton akimtaja kama kocha bora ambaye ameifanya Arsenal kushindana katika mashindano manne kwa wakati mmoja ambayo ni Premier League, UEFA Champions League, FA Cup na EFL Cup.
Kocha huyo alisema soka linapaswa kuwa na mitindo tofauti ya uchezaji, akionya kuwa kama kila timu ingekuwa inacheza kwa mtindo mmoja unaoitwa “mpira mzuri”, basi mchezo ungekuwa wa kuchosha kwa mashabiki na wadau wa soka.
Katika hatua nyingine, Arteta mwenyewe ameendelea kusimama kidete dhidi ya ukosoaji huo wa mbinu za mipira ya adhabu, huku pia akikanusha madai ya kupoteza muda yaliyotolewa na kocha wa Brighton & Hove Albion, Fabian Hürzeler, baada ya Arsenal kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ligi uliochezwa ugenini.

