Licha ya Kukaa Nje Kwa Majeraha, Bajaber Aitwa Harambee Stars

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Mohammed Bajaber, ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Kenya  maarufu kama Harambee Stars kitakachoshiriki michuano ya FIFA Series itakayofanyika mjini Kigali, Rwanda.

Licha ya Kukaa Nje Kwa Majeraha, Bajaber Aitwa Harambee StarsBajaber ambaye bado ni mali ya Simba, amekuwa nje ya uwanja kwa muda baada ya kusumbuliwa na majeraha yaliyomfanya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mara ya mwisho kuonekana uwanjani katika mchezo wa ushindani ilikuwa Januari 18 alipocheza dhidi ya Mtibwa Sugar FC, ambapo alidumu kwa dakika 12 pekee kabla ya kutolewa kutokana na maumivu ya jeraha.

Licha ya Kukaa Nje Kwa Majeraha, Bajaber Aitwa Harambee StarsTangu wakati huo Bajaber amekuwa nje ya mfumo wa kikosi cha Simba huku akiendelea na matibabu na mazoezi maalum ili kurejea katika hali yake ya kawaida ya kimchezo.

Hata hivyo, licha ya changamoto za majeraha, Bajaber bado anahesabika kuwa sehemu ya kikosi cha Simba na anaendelea kufuatiliwa kwa karibu na benchi la ufundi la klabu hiyo.

Licha ya Kukaa Nje Kwa Majeraha, Bajaber Aitwa Harambee StarsWito wa kuitumikia Harambee Stars unaonyesha kuwa bado anaaminiwa na benchi la ufundi la timu ya taifa ya Kenya, huku mashabiki wakisubiri kuona kama ataweza kurejea katika ubora wake na kuisaidia nchi yake kwenye michuano hiyo ya kimataifa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.