Simba Yajipanga Kuivaa TRA United, Barker Asema Kikosi Kiko Tayari

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker amesema kikosi chake kimejipanga vizuri kuelekea mchezo wao wa ligi dhidi ya TRA United, akisisitiza kuwa ushindani wa ligi unahitaji kujitoa kwa kiwango kikubwa ili kufikia malengo ya timu.

Simba Yajipanga Kuivaa TRA United, Barker Asema Kikosi Kiko TayariBarker amesema wanafahamu ugumu wa ligi hiyo na ndio sababu wameweka maandalizi ya kina kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye michezo yao. Ameongeza kuwa Simba inaendelea kuimarika kadri michezo inavyoendelea na wachezaji wanaonyesha ari kubwa ya kupambana.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumzia hali ya kikosi, Barker amesema hakuna mchezaji mwenye majeraha na wote wako tayari kuipambania timu kupata ushindi. “Kikosi chetu kinazidi kuimarika na tunahitaji kuendelea kupata ushindi kwenye mechi zetu. Kuhusu mchezo wetu dhidi ya TRA United tupo tayari na hatuna majeruhi,” amesema Barker.

Simba Yajipanga Kuivaa TRA United, Barker Asema Kikosi Kiko TayariKwa upande wake, mchezaji wa Simba David Kameta amesema wachezaji wamefanya maandalizi mazuri na wako tayari kwa ajili ya mchezo huo, huku wakitarajia kukamilisha maandalizi yao ya mwisho kabla ya kukutana na wapinzani wao.

Simba Yajipanga Kuivaa TRA United, Barker Asema Kikosi Kiko TayariNaye Kocha wa TRA United Etienne Ndairagije amesema kikosi chake kiko tayari kuikabili Simba, akieleza kuwa mchezo huo ni kipimo muhimu kwa timu yake. Mchezaji wa TRA United Nassoro Kapama naye amesisitiza kuwa wachezaji wanatambua ugumu wa mechi hiyo lakini wako tayari kupambana na wapinzani wao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.