Manchester City Yalazimishwa Sare

Klabu ya Manchester City imeshindwa kupata alama tatu muhimu wakiwa katika dimba la nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya goli moja kwa moja na klabu ya Everton.

Vijana wa Pep Guardiola wameshindwa kumaliza mwaka vizuri na hiyo ni kushindwa kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya klabu ya Everton, Ambapo klabu hiyo ilionekana kuumiliki mchezo huo kwa kiwango kikubwa.manchester cityKlabu ya Manchester city waliuanza mchezo kwa kasi kama ilivyo kawaida yao na mapema tu dakika ya 24 Earling Braundt Haaland alifanikiwa kufunga bao la uongozi akipokea pasi safi kutoka kwa Riyad Mahrez, Mpaka mapumziko Man City walikua mbele kwa bao moja kwa bila.

Manchester City walirudi kipindi wakiwa na kasi ileile lakini Everton nao hawakua nyuma kwani walifanikiwa kutengeneza mashambulizi haswa ya kushtukiza, Ndipo mshambuliaji Damai Gray alipofanikiwa kufunga bao la kusawazisha kwa mkwaju mkali dakika ya 64 ya mchezo na kufanya mchezo kua sare ya bao moja kwa moja.manchester cityVijana wa Pep wanadondosha alama mbili ambapo wanakua na alama 36 huku wakiendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini wanaendelea kutngeneza pengo la alama baina yao na vinara Arsenal ambao wana alama 40 na wakifanikiwa kushinda mchezo wao wa siku pengo linaenda mpaka alama saba kutoka alama tano.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.