Kocha msaidizi wa klabu ya Yanga Cedric Kaze amesema klabu hiyo haikucheza vizuri dhidi ya klabu ya Sugar licha ya kupata matokeo ya alama tatu muhimu.
Kocha Kaze wakati anazungumza na waandishi wa habari amesema wanajivunia kupata alama tatu muhimu katika mchezo wa leo lakini hawakucheza vizuri, Klabu ya Yanga imefanikiwa kupata alama tatu katika dimba la Mnungu mkoani Morogoro baada ya kuifunga klabu ya Mtibwa Sugar bao moja kwa bila.
Klabu ya Yanga wanafanikiwa kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 50 kwenye michezo 19, Huku watani zao klabu ya Simba wakiwa nafasi ya pili na jumla ya alama 44.
Klabu ya Yanga imeufunga mwaka ikiwa kileleni na kwasasa nguvu zote wanazihamishia kwenye michuano ya kombe la mapinduzi itakayopigwa visiwani Zanzibar, Huku kocha Kaze akimmwagia sifa kiungo wake Aziz Ki kutokana na uwezo lakini uwezo wake wa kupiga mipira iliokufa na kusema hiyo inatokana na kufanyia mazoezi mara kwa mara.

